Rais Barrack Obama wa Marekani amewasihi wamerakani
wajizue dhidi ya hisia kali baada ya Mmarekani Mweusi kuwapiga risasi na
kuwaua maafisa watatu wa polisi katika shambulizi la pili la kulipiza
kisasi
Rais Barrack Obama
wa Marekani amewasihi wamerakani wajizue dhidi ya hisia kali baada ya
Mmarekani Mweusi kuwapiga risasi na kuwaua maafisa watatu wa polisi
katika shambulizi la pili la kulipiza kisasi dhidi ya polisi wazungu
wanaowaua wamarekani weusi.
Obama ameomba uvumilivu utawale mioyo
ya wakaazi wa mji wa Baton Rouge Louisiana nchini Marekani ambao sasa
wanahofu ya kuzuka mashambulizi ya kulipiza kisasi. Gavin Long ambaye ni mwanajeshi wa zamani aliwapiga risasi polisi kulipiza kisasi mauaji ya Alton Sterling
Obama aliyasema hayo katika hotuba ya moja kwa moja
kupitia kwa runinga kutoka ikulu ya WhiteHouse muda mchache tu baada ya
mtu mmoja mweusi kuua maafisa watatu wa polisi hukohuko Baton Rouge
alikouawa mtu mweusi
Alton Sterling pasi na hatia yeyote majuma mawili yaliyopita. Alton Sterling aliyeuawa na polisi mzungu pasi na kosa lolote
Hasira imekuwa ikitokota miongoni mwa watu weusi
baada ya mtindo wa kuuawa kwa wanaume weusi na polisi wazungu kuendelea
kwa muda mrefu ilihali hakuna hatua inayochukuliwa dhidi yao.
Gavin
Long ambaye ni mwanajeshi wa zamani alikuwa amerekodi ujumbe katika mji
wa Dallas siku chache baada ya polisi watano kuuawa mjini humo katika
shambulizi lililotekelezwa kulipiza kisasi cha mauaji ya Sterling. Hasira imekuwa ikitokota miongoni mwa watu weusi
baada ya mtindo wa kuuawa kwa wanaume weusi na polisi wazungu kuendelea
kwa muda mrefu
Sasa imebainika kuwa Long alikuwa ameweka video
kwenye mtandao akilalamika jinsi polisi wanavyowatendea waamerika weusi
ambapo alitoa wito kwa wanaume weusi kujitolea kuokoa jamii yao.
Long mwenye umri wa miaka 29 aliwahi kuhudumu kama mwanajeshi wa Marekani .
Rais
Obama ameshauri watu weusi dhidi ya kutekeleza mashambulizi dhidi ya
Polisi akisema mauaji ya kulipiza kisasi sio suluhisho la tatizo sugu la
ubaguzi wa rangi bali utachochea uhasama zaidi dhidi yao na polisoi
wazungu.
Post a Comment