Shirikisho la soka
Ulimwenguni (FIFA) limetoa Ratiba ya Kombe la Dunia kwa Klabu ambalo
litadhaminiwa na Alibaba E-Auto na kufanyika huko Japan kati ya Desemba 8
na 18.Mashindano haya yatashindaniwa na Klabu 6 Mabingwa wa Mabara
pamoja na Mwakilishi kutoka Nchi Mwenyeji Japan.
Mechi za
Mashindano haya zitachezwa huko Suita City Football Stadium Mjini Osaka
na International Stadium Yokohama, Mjini Yokohama ambako pia ndipo
itachezwa Fainali .
Hadi sasa Klabu 3 zimeshathibitika kucheza
michuano hiyo ambazo ni Real Madrid, Mabingwa wa Ulaya, waliotwaa
Ubingwa wao Mwezi Mei, na Timu nyingine ni Club America ya Mexico na
Auckland City FC ya Mexico Bara la Oceanic ambazo zilitwaa Ubingwa wao
Mwezi Aprili.
Post a Comment