0

MIDO mpya ya Azam, Enock Atta Agyei aliyekuwa akiichezea Medeama ya Ghana, amesema nafasi ya kwanza kwake kwa timu za Tanzania ilikuwa Yanga kama kocha Hans Pluijm angetaka iwe hivyo lakini matajiri wa Chamazi wakazama kwenye waleti fasta wakafanya yao.

Atta amesajiliwa juzi na Azam kwa mkataba wa miaka miwili na muda wowote

kuanzia jana alitarajiwa kutua nchini ili kujiunga na Azam akitokea Medeama.

Akizungumza na gazeti hili mara ya kumalizika kwa mchezo wa Jumanne kati ya Yanga dhidi ya Medeama, Atta alisema anajuana vizuri na kocha wa Yanga,Pluijm na alikuwa anataka kuzungumza naye ili ampe nafasi.

Kiungo huyo mshambuliaji alisema Pluijm ni moja ya makocha wenye heshima kubwa katika soka Ghana na kila mmoja katika kikosi cha Medeama alitamani pate nafasi acheze katika kikosi cha Mholanzi huyo.

“Alipokuja wiki iliyopita nilitamani nizungumze nae juu ya kuichezea Yanga, lakini nikapata taarifa Azam walishafika kuonana na viongozi wangu, lakini pia nilitaka kumshirikisha katika hili. “Baada ya mazoezi ya mwisho (Jumatatu) nikaambiwa kuwa viongozi wapo hatua za mwisho kukamilisha uhamisho wangu kujiunga Azam, nikaona si jambo baya lakini nilitaka bado kumshirikisha kocha Pluijm,” alisema.

Wachezaji karibu wote wa Medeama walimkimbilia Pluijm mara baada ya kushangilia ushindi wao na walitumia muda mwingi kuzungumza nae.

Nahodha wa Medeama, Kwakwa alisema Pluijm ana nafasi kubwa ya kumsajili

mchezaji yeyote Medeama kama Yanga itakuwa na uwezo wa kuvunja mikataba yao kutokana na kujulikana zaidi na vijana wanaocheza soka kwa sasa.

Kwa upande wake, Pluijm alisema anawafahamu karibu nyota wote wa Medeama kutokana na kuwafundisha soka wengi wao wakiwa bado vijana wadogo wakicheza soka katika timu za vijana.

“Ni kweli, wengi nimewafundisha soka na nawajua vizuri hivyo hata sina presha, nimejaza nafasi za kusajili nyota wa kimataifa lakini naweza kumsajili yeyote katika kikosi chao,” alisema Pluijm.

Yanga ilikuwa nchini Ghana katika mchezo wake wa Kombe la Shirikisho Afrika waliopoteza kwa kuchapwa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji wao, Medeama baada ya sare ya 1-1 mechi ya awali.

Post a Comment

 
Top