WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema Serikali
inasubiri Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC) naTume ya Uchaguzi Zanzibar
(ZEC) zimalize majadiliano ili mchakato wa kuipigia kura ya maoni Katiba
Inayopendekezwa ufanyike.
Waziri Mwakyembe alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana alipokutana na uongozi wa Kikosi cha Kupambana na Haki za Mirathi (Kikuhami ) kilichoko chini ya Chama cha Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WiLDAF).
Alisema kura hiyo ya maoni ingekuwa imeshafanyika lakini Tume za Uchaguzi ziliona ni bora iahirishwe kwanza ili kupisha nchi kukamilisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
Alisema kukamilika kwa Uchaguzi Mkuu kunatoa fursa kwa Serikali kuendelea na mpango wake wa kuendesha kura ya maoni juu ya Katiba Inayopendekezwa ili kupata Katiba Mpya ya Tanzania.
Aliongeza kuwa Katiba Inayopendekezwa ina vitu vingi sana ambavyo vitasaidia upatikanaji wa haki za wanawake na kuondoa uonevu dhidi yao na hivyo kufanikisha harakati ambazo wadau mbalimbali wanawake nchini wamekuwa wakizipigania na hivyo kukamilika wakati Katiba Mpya itakapokuwa imepatikana.
Aidha Waziri aliutaka uongozi huo wa Kikuhami kupitia WiLDAF kuwasilisha wizarani mapendekezo yao juu ya mabadiliko ya sheria mbalimbali za mirathi nchini wanazoziona zinawakandamiza wanawake ili ziweze kufanyiwa marekebisho na ziendane na wakati uliopo.
Kikuhami chini ya uongozi wa Thabita Siwale ulimuomba Waziri Mwakyembe kuangalia uwezekano wa kuondoa sheria zinazowakandamiza wanawake hasa zile za mirathi.

Post a Comment