0

Dar es Salaam. Kapteni  wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), P 12531 Henrick Mahenge (34) mkazi wa Mlimani City, Dar es Salaam amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala leo kujibu mashtaka ya kujaribu kumuua askari wa usalama barabarani.

Kapteni Mahenge ambaye ni mkazi wa Mlimani City,  amepandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan na kusomewa shtaka linalomkabili.

 Akisoma mashtaka, Wakili wa Serikali, Grace Mwanga amedai mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai 12, mwaka huu maeneo ya Mnazi Mmoja wilayani Ilala.

 Mwanga alidai kuwa kuwa mshtakiwa alijaribu kumuua  kujaribu kumuua askari wa usalama barabarani WP  5177  Clesensia Makanyaga.

Mshitakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo.

Hata hivyo, Mwanga alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kwamba hali ya mgonjwa haijulikani hivyo aliomba mahakama izuie dhamana hadi watakapopata uhakika kuhusu hali ya mgonjwa.

Mshtakiwa alipopewa nafasi ya kuelezea kilichotokea, alidai hakutishia kuua na kwamba, yeye ndiye alifanyiwa fujo na kuchaniwa nguo zake.

Alidai alimuona mshitakiwa baada ya tukio na kwamba hakupata taarifa kuwa mlalamikaji yupo hospitali.

Hakimu Hassan alisema kuwa dhamana ipo wazi kwa wadhamini wawili kutoka taasisi zinazotambulika na kuwataka wakaguliwe kwanza kujiridhisha.

 Hata hivyo, alisema mshtakiwa arudi rumande hadi Julai 19, mwaka huu watakapojiridhisha na wadhamini pamoja na kujua hali ya mlalamikaji.

Post a Comment

 
Top