0

Serikali ya Tanzania imekabidhi Malaysia kipande cha bawa la ndege kilichookotwa na wavuvi eneo la la Kojani Kisiwani Permba amabalo linaaminika ni kutoka kwenye ndege ya Malaysia iliyopotea miaka miwili iliyopita.

Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika makao makuu ya mamlaka ya usafiri wa ndege jijini Dar es salaam T.C.A.A. kati ya katibu mkuu wa wizara ya ujenzi uchukuzi na mawasailiano Dk, Leornard Chamuroho na Balozi wa Australia kwa eneo la Afrika mashsriki John Feakes.

Uchunguzi wa mabaki ya ndege ya Malaysia MH 370 iliyopotea mwaka 2014 na kupoteza zaidi ya abiria 274 wakati ikitokea jijini Kuala Lumpur kuelekea Beijing China unafanyika nchini Australia.

Juni 20 mwaka huu mvuvi mmoja katika kisiwa cha Kojani Pemba alioona bwawa hilo la ndege na kutoa taarifa kwa mamlaka zinazohusika.

Post a Comment

 
Top