Moja ya habari zilizoandikwa kwenye magazetini hii kwenye gazeti la Mtanzania yenye kichwa cha habari ‘Facebook sasa kutuma na kupokea fedha bure’
Gazeti
hilo limeandika kuwa utandawazi unazidi kushika kasi ambapo kadri siku
zinavyozidi kwenda mambo yanabadilika. Ndiyo maana sasa hivi kuna mambo
mengi ambapo licha ya kuwa Tanzania mambo mengine yanachelewa kutufikia,
lakini siku moja tutatumia huduma hizo kama ilivyo kwa mataifa
yaliyoendelea kiteknolojia.
Kila
kukicha mmiliki wa mtandao huo, Mark Zurgbeck amekua na mawazo mapya ya
kuvutia kwa wateja kwenye huduma yake hiyo kwa kubuni mambo mbalimbali
yanayowagusa wateja wake.
Kama wewe
ni miongoni mwa wanaotumia mtandao huu kupitia App ya Messenger tambua
kuwa siku chache zijazo utakua na uwezo wa kufanya malipo ya bidhaa au
kutuma na kupokea fedha kupitia mtandao huo.
Huduma hiyo iliyobatizwa jina la PayPal
itakua ikitumika kama ilivyo ile ya simu japo cha kufurahisha hapa ni
kuwa huduma hiyo haitakuwa na makato ya aina yoyote kama ilivyo kwa
mitandao ya simu, isipokuwa tu itawahusu watumiaji wa Debit Card pekee
na walio na umri wa miaka 18 na kuendelea.
Huduma hiyo itaanza kutumika nchini
Marekani ambapo mtu atatuma na kupokea fedha huku ikitarajiwa kusambaa
kwenye mataifa mengine.
Namna ya kutumia huduma hii fungua
sehemu yako ya Chatting kisha chagua More halafu nenda kwenye alama ya $
halafu nenda palipoandikwa ‘Pay’ kisha unamalizia na sehemu
iliyoandikwa ‘Add New Debit Card kisha utaulizwa kiasi unachohitaji
kulipia utaingiza na kuletewa risiti
Post a Comment