Donald Trump
ateuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican, uchaguzi
unaotarajiwa kufanyika mwezi November mwaka huu. Trump amepata uungwaji
mkono na wajumbe kutoka majimbo na wilaya za Marekani katika kura
mchujo wa kumpata mgombea wa nafasi hiyo kupitia chama chake cha
Republican kupitia mkutano mkuu wa chama chake mjini Cleveland.
Baada
ya kuchaguliwa kuwa mgombea urais Donald Trump alitoa shukran zake
kupitia mtandao wa twitter,na imetanabahishwa kwamba gavana wa jimbo la
Indiana Mike Pence, ndiye mgombea mwenza .Taarifa zaidi zinasema watoto
wawili wa Donald Trump wa kiume Donald na pia bintiye Tiffany
wanatarajiwa kuhutubia mkutano mkuu wa wanachama wa chama hicho .
Post a Comment