0
Mbwa anayechapa zoezi kali
Je wewe hufanya mazoezi ya kuboresha afya yako kila siku ?
Amini usiamini , nchini Uingereza kuna mbwa anayefanya mazoezi na kutunisha misuli ya miguu na mikono kwa mpia kila siku
Jibwa la polisi nchini Uingereza limewashangaza watu wengi.
Jibwa hilo lilijiunga na afisa wa polisi Steve Hopwood kutoka kituo cha polisi cha Avon Somerset kufanya mazoezi .
Mbwa huyo hupiga ''Pressups'' 22 kila siku.
Yaani mbwa huyo aina ya German Shephered anaweza kutunisha misuli mara 22 kwa mpigo kila wakati akifwata maagizo ya afande Hopwood.
Mbwa huyo anajiunga na afande Hopwood katika ''22PressUps Challenge'' kwa nia ya kuhamasisha umma na serikali kuhusiana na ongezeko la idadi ya maafisa wanaojitia kitanzi baada ya kustaafu kazini.

Post a Comment

 
Top