July 28 2016 katika mitandao ya kijamii na vyombo
vya habari ilikuwa ni pamoja na hii ya kutokea nchini India
iliyohusu kifo cha mpiga picha wa Gazeri la Tanzania Daima Joseph Senga aliyefariki akiwa katika matibabu ya ugonjwa wa moyo.
Marehemu Joseph Senga ndiye mpiga picha aliyenasa tukio la mauaji ya Mwandishi wa habari wa kituo cha talevisheni CHANEL 10 Daud Mwangosi kilichotokea September 2 2012 katika kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Leo July 30 2016 mwili wa marehemu Joseph Senga tayari umewasili nchini ukitokea India, ambapo Waziri wa habari, utamaduni sanaa na michezo Nape Nnauye aliungana na baadhi ya watanzania wakiwemo wapiga picha wenzake wa kutokea vyombo mbalimbali vya habari.
Tayari nimekusogezea picha 6 kutokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es salaam
Waziri Nape Nnauye na wananchi wakishirikia kubeba jeneza
Baadhi ya wapiga picha wakiongozwa na Loveness Bernard wakiwa katika vazi la pamoja
Wapiga picha kutokea vyombo mbalimbali vya habari walipokuwa wakiusubiri mwili wa marehemu
Picha zote na Othman Michuzi
Post a Comment