Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI), George Simbachawene (Mb), Katikati akizungumza wakati wa
ziara ya kukagua mradi wa mabasi yaendayo haraka leo jijini Dar es
Salaam.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kushirikiana na viongozi wa Mkoa huo kuhakikisha kuanzia leo hakuna mfanyabiashara atakayefanya biashara katika maeneo ya makutano ya barabara na katikati ya jiji.
Pia amemtaka Makonda kuhakikisha anawaondoa ombaomba wote walipo katika makutano hayo pamoja katikati ya jiji kuweza kusaidiwa na sio kuomba hawawezi kujikwamua na umasikini.
Simbachawene alitoa agizo hilo leo alipofanya ziara katika mradi wa Mabasi yaendayo haraka UDART na kudai kwamba bado kuna changamoto kubwa kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri kutokana na watu kushindwa kufuata sheria ambazo zimewekwa.
Amesema lengo la kuwaondoa wafanyabiashara na ombaomba hao ni kutaka kuhakikisha kwamba jiji la Dar es Salaam linakuwa katika muonekano mzuri na usafi na kuweza kufuta mbinu nyingine ya kuwasaidia kupitia mfuko wa TASAF.
"Kuanzia leo sitaki kumuona mfanyabiashara katika maeneo hayo ya makutano na pembezoni mwa barabara watafutieni utaratibu ambao utawafanya wakae maeneo salama kutokana kila manispaa ilivyoanisha "amesema Simbachawene.
Aliongeza kuwa anataka katika maeneo hayo kuwepo na askari saa 24 ambao watahakikisha hakuna mfanyabiashara atakayefanya biashara baada ya kuondolewa.
"Acheni kukamata mama ntilie nataka askari hao watumike kuwakamata wafanyabiashara hao wakae hapo saa 24" amesema Simbachawene.
Amesema kuongezeka kwa uchafuzi wa mazingira katika maeneo ya jiji kunachangiwa na uwepo wa biashara zinazofanywa katika mazingira ambayo sio rasmi na ndia chazo cha uchafu.
Kwa upande wa usafiri wa Mabasi yaendayo haraka UDART,Simbachawene pia amewataka wamiliki wa vyombo vya usafiri kufuata sheria na kuacha kutumia Barabara za mwendo haraka hususani pikipiki na maguta.
Amesema serikali imejipanga kukabiliana na changamoto foleni kusimamia utekelezaji wa barabara za mabasi ya mwendo wa haraka awamu ya pili unatarajia kuanza mwakani.
Simbachawene amesema tayari wameshafanya tathimini na utatumia miaka miwili hadi kukamilika kwake pia wapo katika mchakato wa kumtafuta mkandarasi kwaajili ya ujenzi.
Amesema awamu ya pili itaanzia katika Barabara ya sokoine kuelekea barabara ya Kilwa hadi Mbagala na kutakuwa na barabara za juu katika makutano ya barabara ya Kawawa na Nyerere,
Nae Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amemuahidi Waziri huyo kuwa watatekeleza maagizo yote na kuahidi kuanzia oparesheni hiyo leo.

Post a Comment