Baadhi
ya wananchi katika mkoa wa Kagera wamepongeza serikali ya awamu ya tano
iliyo chini ya rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutenga kiasi cha
fedha kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 kwa ajili ya ununuzi wa
meli mpya mbili zitakazotoa huduma ya usafiri ndani ya ziwa Victoria na
kuzifanyia matengenezo makubwa meli zilizosimamisha huduma kutokana na
ubovu za MV.Serengeti na MV. Victoria.
Wananchi hao wakizungumza na Waandishi wa habari kwa nyakati tofauti wakati wakitoa
pongezi kwa rais huyo wamesema uamzi wa serikali ya awamu ya tano wa
kutenga bajeti ya kununua meli mpya na kukarabati meli mbovu
unamdhihirisha wazi rais wa awamu hiyo alivyo na mapenzi ya dhati kwa
wananchi waliomchagua kwa kuwa baadhi ya marais wa serikali za awamu
zilizopita walitoa ahadi za ununuzi wa meli bila kuzitimiza.
Kwa upande wake Abdul Ziadi, mwenyekiti wa watoa huduma katika
bandari ya Bukoba amesema kusimamishwa kwa meli za MV. Serengeti na MV.
Victoria kuwa kumewaathiri sana wananchi wengi waliokuwa wakitegemea
safari za meli hizo katiika kujipatia kipato na katika kusafirisha
bidhaa zao hivyo akaeleza kuwa dhamira ya Dkt. Magufuli ya kununua meli
mpya na kutengeneza zile za zamani kuwa inapaswa kupongezwa na kila mtu.
Mv. Serengeti ndio ilikuwa meli pekee iliyokuwa ikitoa huduma za
usafiri ndani ya ziwa kati ya bandari ya Bukoba na Mwanza ilisimamisha
Machi 21, mwaka huu kutokana na ubovu, usafiri wa meli hiyo kila wiki
ulikuwa ikiingia kampuni ya taifa ya huduma za meli zaidi ya shilingi
milioni 36.
Post a Comment