Wakazi
wa kijiji cha Manga kilichopo kata ya Mkata wilayani Handeni wameiomba
serikali kuingilia kati kufuatia walimu wawili wa shule ya msingi
Kwedichocho kuacha kazi tangu mwishoni mwa jana na kuwaacha wanafunzi
wakifundishwa na wanafunzi wenzao wawili wa darasa la saba kufuatia
vitongoji vyao pamoja na shule kuuzwa kwa mwekezaji ikidaiwa kuwa ipo
maeneo katika kijiji kingine kinachojulikana kwa jina la Mazingara.
Wakizungumza katika kijiji cha Kwedichocho baadhi ya viongozi wa
serikali ya kijiji na wakazi wake wamesema hatua hiyo imekuja baada ya
baadhi ya viongozi wa kijiji cha Mazingara kumuuzia mwekezaji hekari
zaidi ya 400 zenye makazi ya watu zaidi ya 1000 pamoja na shule hatua
ambayo wanafunzi wameanza kutishiwa kuondoka kwa sababu mwekezaji
anataka kulifanyia kazi eneo la ardhi ikiwa ni pamoja na majengo ya
shule pamoja na nyumba ya mwalimu.
Kwa upande wake mwenyekiti mstaafu wa kijiji hicho Saleh Sadick
amesema wakazi wa vitongoji vya Kwedichocho na Mkulumilo vyote vilivyopo
katika kata ya Mkata hawatakubali kuondoka katika eneo hilo linalodaiwa
kuwa ni eneo la kijiji cha Mazingara hatua ambayo inaweza kusababisha
uvunjifu wa amani baina ya pande hizo mbili.
ITV ilifika hadi katika shule ya msingi Kwedichocho ambapo
wananfunzi walikutwa darasani wakifundishwa na wenza wa darasa la saba
huku wakiimba wimbo unaosema bado mapambano yanaendelea.
Post a Comment