Na Daudi Manongi,MAELEZO.
Mkurugenzi
Mkuu Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya Bw.Godlove Mbwaji amehaidi
kufanya kikao na uongozi wa waendesha bodaboda wa mkoa wa mbeya ili
kuzungumzia suala la waendesha pikipiki hao kuvamia hospitali hiyo
wakiwa katika kundi kubwa wakati wanapofiwa na dereva mwenzao na
kusababisha usumbufu kwa wagonjwa na wakazi wa mbeya.
Mkurugenzi
uyo ametoa rai kwa waendesha bodaboda hao kuwa na nidhamu wanapoingia
katika hospitali hiyo kwani inatumiwa na wakazi wote wa Jiji la Mbeya na
husababisha hatari kwa wagonjwa wanaohitaji huduma ya dharura hospitali
hapo kwani huziba barabara yote.
Aidha
ameuomba uongozi wa waendesha bodaboda hao kuchagua watu wachache
wanapokuja kuchukua mwili wa mwenzao kwani itasaidia kupunguza kelele za
honi na vyombo vyenyewe kwani pia kuna majirani wanaokaa katika eneo
hilo wanatumia barabara hizo na hivyo kuepusha ajali.
Pia
Bw.Mbwaji ametoa ushauri kwa uongozi wa waendesha bodaboda hao kuacha
vitendo vya uvunjifu wa sheria na wafuate Sheria,Kanuni na taratibu za
Barabarani pale mmoja wapo anapokamatwa au kugongwa kwa kutojicjhukulia
sheria mkononi kumpiga aliyemgonga au kuwafanyia fujo polisi kwa
kumvamia muhusika wakiwa katika makundi makubwa na hivyo kuhatarisha
usalama wa Raia.
Aidha
baadhi ya madereva bodaboda wa mkoa huo wamesema kuwa wamekuwa
wakishinikizwa na viongozi wa matawi yao kwa madai kuwa atakayekataa
kwenda kwenye maandamano atatozwa faini ya sh.50000, hata kama amebeba
abiria ulazimishwa kumshusha.
Post a Comment