Mwenyekiti wa chama
cha mpira cha Uingereza, Greg Dyke amewaandikia barua chama cha
shirikisho la soka barani Ulaya,UEFA kutoa maelezo ya tija kuhusu
mpangilio wa ulinzi wakati wa michuano ya soka ya Euro 2016.
Leo
Urusi itacheza katika mji wa Lile ambapo mashabiki wa Uingereza pia
watakusanyika hapo kwa kuwa mechi yao itakuwa kesho.
Kulikuwa na
usumbufu mkubwa katikati hapo wakati timu zote zilipopangwa mwishoni mwa
juma.Mashabiki sita wa England wamefungwa kutokana na vurugu
zilizotokea lakini hakuna yeyote kati ya mamia ya mashabiki wa Urusi
aliyewekwa hatiani,Maafisa wa Ufaransa wameliita tukio hilo kuwa ni
vurugu za kihuni,hivyo timu zote mbili zilipaswa kutolewa katika
michuano kama patatokea vurugu nyingine.
Post a Comment