Maafisa wakuu
nchini Uganda wanasema kuwa walinda usalama wamekabiliana vikali na
kundi moja la watu, waliokuwa wamejihami kwa silaha, waliojaribu kuvamia
kituo cha polisi kilichoko katikati mwa Gulu.
Gulu ni mji ulioko kaskazini mwa Uganda.
Polisi
inaamini kuwa shambulio hilo lilikuwa njama za kujaribu kumuokoa
mwanasiasa mmoja wa upinzani anayezuliwa- Dan Oola Odiya.
Wanasema kuwa milio ya risasi ilidumu kwa muda wa dakika thelathini.
Taharuki ya kisiasa imetanda nchini Uganda, kufuatia matokeo tata ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Februari mwaka huu.
Juma
lililopita, jeshi la Uganda liliwatia mbaroni askari thelathini na raia
kadhaa, likisema kuwa walikuwa na njama ya kuunda kundi la waasi.
Post a Comment