Rais wa nchi za
Umoja wa Ulaya wanaotumia sarafu ya Euro, Jeroen Dijsselbloem, amesema
sasa taasisi za kifedha za Uingereza zitakuwa na mahusiano machache tu
na zile za kifedha za Muungano wa Ulaya baada ya taifa hilo kuondoka
rasmi kutoka kwa jumuiya hiyo.
Bw. Dijsselbloem amekiambia kituo
cha televisheni cha Uholanzi kuwa hali hiyo itayalazimu baadhi ya
makampuni kuhama mji wa London.
Waziri wa fedha wa Uholanzi kwa
upande wake amesema anatarajia miji ya Frankfurt na Amsterdam kufaidika
kibiashara kutokana na msukumo huo utakaojiri wa biashara kulazimika
kuhamia kwengineko Ulaya ili kutoroka masharti magumu ya kazi
yatakayoikumba Uingereza baada kujitoa kutoka EU.
Post a Comment