Mataifa 6
waanzilishi wa Muungano wa Ulaya EU wanakutana leo kujadili mustakabali
wao wa baadaye baada ya Uingereza kuamua kujiondoa kutoka kwa muungano
huo.
Mawaziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, ufaransa,Italy,
Ubelgiji, Luxembourg na Uholanzi wanatarajiwa kuanzisha mchakato huo
pasi na kuwa na ngoja ngoja.
Tayari rais wa tume ya muungano wa
Ulaya , Jean-Claude Juncker, amesema anataka kuanzisha majadiliano mara
moja ya jinsi Uingereza itakavyotoka rasmi kutoka EU .
Bw.Juncker amesema haieleweki kwamba swala hilo
likumbwe na hadi waziri mkuu wa Uingereza David Cameron, ang'atuke
kutoka madarakani baada ya kushindwa katika kura hiyo ya maoni iliyoamua
nchi hiyo ijibandue kutoka Umoja wa Ulaya.
Mawaziri hao pia
wanatarajiwa kuweka masharti mapya yatakayowazuia wanachama wengine
kuiga mfano wa Uingereza,baada ya vyama vya mrengo wa kulia katika
mataifa mengi duniani kupongeza uamuzi huo wa Uingereza kujitoa kutoka
muungano wa Ulaya...
Hata hivyo waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani
Frank-Walter Steinmeier, amewatahadharisha wenzake kutokuwa na hamaki na
kutaka kuchua hatua za kama kuilipizia kisasi Uingereza .
Ameomba
kuwepo kwa subra na umakini katika kulishughulikia swala hilo ambalo
anasema linapaswa kuongozwa tu na vipi kushughulikia mahitaji ya raia wa
jumuiya ya muungano wa Ulaya.
Post a Comment