0

Dodoma. Bajeti iliyosomwa jana na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango inaonekana kuwa mwisho wa makomandoo ambao hujinufaisha na mapato ya milangoni, tiketi feki na uuzwaji wa vishina vya tiketi katika viwanja vya soka nchini.

Akisoma bajeti ya Serikali bungeni mjini Dodoma jana, Dk Mpango alisema Serikali imekabidhi mamlaka ya kukusanya mapato yasiyo ya kodi ikiwamo kodi ya majengo kwa Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA).

 “Miongoni mwa makusanyo yanayolengwa ni tozo, faini kama vile za Mahakama na usalama barabarani, ada, viingilio kwenye hifadhi za Taifa, viwanja vya michezo  na vibali vya kuvuna maliasili,” alisema  Dk Mpango.

Post a Comment

 
Top