Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta amesisitiza kuwa serikali haitaruhusu
maandamano ya ghasia akitaja yale yanayofanywa na chama cha Upinzani
Cord ambayo yamegeuka na kuwa maandamano na maafisa wa polisi.
Lakini aliongezea kuwa wataruhusu maandamano iwapo yatasalia kuwa ya amani kama ilivyo katika katiba.
Upinzani wa Cord umekuwa akifanya maandamano mara kwa mara ukitaka mabadiliko katika tume ya uchaguzi.
Awali siku ya Ijumaa upinzani huo umesema utakiuka agizo la waziri wa usalama la kupiga marufuku maandamano.
Bw Kenyatta ameutaka upinzani kuzungumza na serikali kuhusu maswala muhimu.''Tumetengeza timu... yetu leteni yenu'',alisema.
Post a Comment