0


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda atazindua maonyesho ya kwanza ya simu original katika viwanja vya Posta jumamosi ya Tarehe 11 mwezi huu kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 12 jioni.

Lengo kuu la kufanyika kwa maonyesho hayo ni kuwapa elimu wateja wa simu kujua ipi ni simu fake  na ipi ni original kutoka kwa makampuni hayo ya simu,pia kwa kushirikiana na TCRA watatoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya simu na mitandao ya kijamii.

Lengo la tatu ni kuhakikisha wateja wanajipatia simu original kwa bei nafuu kabla ya simu fake kuzimwa tarehe 16 mwezi huu.

Nae Kaimu Katibu mtendaji wa Baraza la watumiaji wa huduma za mawasiliano(TCRA-CCC),Mary Msuya amewashauri watumiaji wa simu nchini kununua simu katika maduka ya simu na kuomba risiti ya dhamana ya muda wa matumizi ya bidhaa usiopungua miezi 12.

Aidha aliwataka wafanyabishara wasio waaminifu kuacha mara moja kuingiza bidhaa feki nchini kwa njia za panya kwani serikali iko makini katika kusimamia suala hilo.

Kwa upande wake mwakilishi wa makampuni ya simu Meneja mauzo wa kampuni ya Tecno Bw.Fred Kadilana ametoa wito kwa watumiaji wa simu kuja kwa wingi ili kujipatia simu zenye ubora wa hali ya juu kutoka kampuni mbalimbali.

Wateja wa simu za mkononi watajipatia simu original kutoka katika maonyesho hayo kwa bei nafuu kutoka kwa makampuni ya simu ya Samsung,Tecno,Startimes,Huawei na Itel uku kukiwa na ushiriki wa makampuni ya simu ya Vodacom,Tigo na TTCL.

Katika maonyesho hayo Taasisi mbalimbali za serikali zitashiriki kama mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano (TCRA-CCC) na Mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF).

Post a Comment

 
Top