Taarifa kutoka
Libya zinasema kuwa miili ya watu wanaodaiwa kuwa ni wahamiaji,
imepatikana ikiwa imetapakaa katika mwambao wa bahari karibu na mji wa
Zuwara.
Baadhi ya taarifa zinasema zaidi ya miili 85 imeonekana
ikiwa imetapakaa. Ofisa kutoka shirika la msalaba mwekundu nchini humo
anasema miili hiyo inahisiwa kwamba huenda ni ya watu kutoka ukanda wa
jangwa la Sahara.
Hata hivyo imekuwa ni vigumu kujua kwamba ni lini hasa watu hao walizama.
Eneo linalozunguka mji wa Zuwara ni miongoni mwa sehemu za pwani ya Libya ambazo wahamiaji huanzia safari zao kuelekea ulaya.
Post a Comment