Uingereza wamekamlisha maandalizi
yao ya Euro 2016 kwa ushindi mwembamba dhidi ya Ureno iliyocheza ikiwa
na watu kumi katika dimba la Wembley.
Chris Smalling alimalizia
kwa kichwa mpira uliopigwa na Raheem Sterling aliyeingia kutoka benchi
na kuandika bao hilo la pekee. Timu ya Ureno ilicheza pungufu kutokana
na mlinzi wake wa kati Bruno Alves kuonyeshwa kadi nyekudu baada ya
kumchezea madhambi mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane dakika ya 35.
Jambo pekee la kufurahisha kwa Hodgson ni kwamba wachezaji wake wote
wapo tiyari kiafya kushiriki michuano ya Euro 2016.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment