Mbunge wa Korogwe Vijijini Steven
Hillary Ngonyani ‘Maji Marefu’ amesema anaunga mkono hatua ya serikali
kuongeza kodi kwa watu wote wanaoweka majina yao kama ‘Plate Number’ ili
fedha hizo zisaidie wananchi wengine.
Ngonyani ameyasema hayo baada ya hotuba
ya Waziri wa fedha Philip Mpango kuonyesha kwamba kwa watu wanaotaka
majina yao yawe Plate Number watalipia milioni 10 kama kodi kutoka
milioni 5 za awali.
”Mimi naona ni kitu cha kawaida kwa
kuwa haiingiliani na namba za serikali hivyo hata wangeweka milioni 20
ni sawa tu ili kuwafanya vijana wanaotaka umaridadi waweze kuchangia
serikali”
Aidha Mbunge huyo ameipongeza serikali
kwa bajeti nzuri ambayo amesema imegusa maisha ya watu wa chini kwa
kujali miradi ya barabara, reli, ndege na bandari.
Post a Comment