Msanii mashuhuri wa
filamu nchini Marekani, Will Smith na aliyekuwa bingwa wa dunia wa
uzani wa juu Lennox Lewis, wameteuliwa kuwa miongoni mwa watu
watakaobeba jeneza la bondia bingwa mara tatu duniani marehemu Muhammed
Ali.
Mwaka wa 2001 Smith aliigiza katika filamu kumhusu Muhammad Ali kama Ali, jambo lilimsababisha kuteuliwa katika tuzo la Oscar.Tangu hapo amekuwa rafiki wa familia hiyo ya Muhammad Ali.
Lewis kwa upande wake ni miongoni mwa mabondia watatu kwa pamoja na Ali na Evander Holyfeild ambao wamewahishinda taji la uzani wa juu mara tatu.
Wawili hao sasa wataungana na jamaa na marafiki kuubeba jeneza la Ali, mjini Kentucky siku ya Ijumaa wakati wa mazishi yake.
Ali alifariki siku ya Ijumaa mjini Arizona alikokuwa amelazwa hospitalini akiwa na umri wa miaka 74.
Post a Comment