Karibu wapiganaji
50 wanaoamika kutoka kundi la Lord's Resitance Army (LRA) la nchini
Uganda, waliendesha uvamizi mishoni mwa wiki katika eneo lililo umbali
wa kilomita 500 kaskazini mwa mkoa wa Kisangani nchini Jamhuri ya
Demokrasi ya Congo.
Karibu watu 100 wanaaminika kutekwa nyara
wakati wa uvamizi huo. Wale waliotekwa wanaripotiwa kulazimishwa kubeba
mali ambayo wapiganaji hao walikuwa wamepora.
Wanafunzi ambao
walikuwa wamesafiri kutoka vijiji vilivyo karibu kuja kufanya mtihani wa
kitafa wa shule ya msingi, wakiwemo wafanyibiashara na wauguzi
waliokuwa wakitoa chanjo dhidi ya ugonjwa wa uti wa mgongo, ni kati ya
wale waliotekwa nyara.
Usimamizi wa eneo la Bondo ambapo kisa
hicho kilitokea, unasema kuwa wanajeshi wamewafuata wapiganaji hao
kwenda msitu wa Adama yaliko maficho yao.
Kundi la LRA
lilianzishwa nchini Uganda karibu miongo mitatu iliyopita, lakini
likahamia nchi zingine majirani kutokana oparesheni iliyokuwa
ikiendeshwa na jeshi la Uganda.
Post a Comment