0

                              

Serikali imesema imetenga shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya kuanzisha mahakama ya mafisadi katika mwaka wa fedha 2016 & 2017 ikiwa ni ahadi ya Rais Dkt. John Magufuli wakati wa kampeni uchaguzi mkuu 2015.

Hayo yameelezwa Bungeni Dodoma wakati Waziri wa Fedha Dkt. Philip Mpango akisoma bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016 & 2017.Pia serikali imetenga Bilioni 72.3 kwa ajili ya kuiwezesha TAKUKURU kukabiliana na rushwa iliyoshamiri katika maeneo mengi nchini.

Aidha kwa upande mwingine serikali imetenga shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kukabiliana na migogoro ya ardhi ambayo imejikita katika maeneo mengi ya wakulima na wafugaji.

Bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016 & 2017 ni jumla ya shilingi Trilioni 29.5 matumizi ya kawaida ni Trilioni 17.7,

Hata hivyo wakati wa kusomwa kwa bajeti hiyo wabunge wa upinzani wamesusia kikao hicho kwa madai ya kutokuwa na imani na Naibu Spika Tulia Ackson.

Post a Comment

 
Top