Magari mengi ya usafiri jijini
Nairobi, Kenya, maarufu kama "matatu" yana kunguni, kwa mujibu wa gazeti
la standard la nchi hiyo.
Kondakta mmoja anaripotiwa kuliambia
gazeti la Standard, kuwa wadudu hao wanatishia kuharibu biashara ya
kutoka na sababu kuwa watu wengi uhofia kupanda "Matatu"Wadudu hao husambazwa na wateja kutoka kwa nyumba zao bila kujua, ambao kisha hubaki kwenye viti vya magari.
Sasa wahudumu wa sekta ya usafiri jijini Nairobi, wameanzisha kampeni ya kuangamiza kungunu hao kwa kunyunyiza dawa na pia kuwataka abiria kutoa habari ikiwa wataona wadudu hao.
Post a Comment