0
                
Liwale super cup leo june 23 kulikuwa na mchezo kati ya Kigamboni fc Vs Likombora fc,mchezo uliochezwa uwanja wa wilaya ya Liwale.

 Katika kipindi cha kwanza Kigamboni fc iliongoza goli 3 Magoli Yaliofungwa na Fides chalesi dakika 30, Rehemani mtipa dakika 37 na Shadhili kimbowe dakika 44 kwa mkwaju wa penaiti.

 Kipindi cha pili kigamboni fc waliongeza goli lililofungwa na Rehemani mtipa dakika 59 Na Likombora fc walifunga goli 2 zilizofungwa na Saidi kipinga dakika 48 Abdala kiindikwa dakika 86 kwa mkwaju wa penaiti.

Matokeo ya mchezo wa leo Kigamboni fc 4-2 likombora fc 

Kocha wa Kigamboni fc bwana Faraji Ngalinga alisema ushindi kwao ni kawaida ila haitaibeza timu yeyote na kocha wa Likombora fc bwana Mauridi Kijagi alisema mchezo ulikuwa mzuri lakini tatizo likuwa katika maandalizi hayakuwa mazuri ila anamatumaini ya mchezo ujao atashinda.

Ratiba ya ligi Liwale super cup

 Kundi A 
  1.  Sido fc
  2.  Polisi fc 
  3. Transporter fc
  4.  Kipule fc
  5.  Mnarani fc 
 Kundi B 
  1.  Kigamboni fc 
  2. Mpengele fc 
  3. Likombora fc 
  4.  Likongowele city fc 
 Group C
  1.  Hawili fc 
  2. Nangando city fc 
  3. Mihumo fc Liwale B fc 
  4. Liwale B fc


 June 24 2016 kutakuwa na mchezo Hawili fc Vs Liwale B fc

Post a Comment

 
Top