0
Sweden 
Italia walifunga bao dakika ya 88
Timu ya taifa ya Italia imefika hatua ya muondoano katika michuano ya ubingwa wa Ulaya baada ya kujipatia ushindi dhidi ya Sweden.
Ushindi wa Italia ulitokana na bao la pekee la mechi hiyo, lililofungwa na Eder dakika za mwishomwisho.
Ishara zilionesha kana kwamba mechi hiyo ingemalizika sare tasa hadi pale Eder alipokimbia na kufikia mpira kutoka kwa Simone Zaza nje kidogo ya eneo la hatari dakika ya 88.
Sweden hawakupata kombora hata moja la kulenga goli kwa mechi ya pili mtawalia.
 
Mshambuliaji nyota Zlatan Ibrahimovic alinyamazishwa mechi yote.
Italy wanaongoza Kundi E na alama sita. Sweden wamo nambari tatu na alama moja.

Post a Comment

 
Top