0


Ugaidi ni mfumo wa kulenga mabadiliko ya kisiasa kwa kutisha watu kwa njia ya vurugu au mauaji. Matendo ya kigaidi yanatisha kwa sababu watu wanajeruhiwa au kuuawa. Watendaji wa ugaidi kwa kawaida ni vikundi au watu wasio na cheo au nafasi rasmi.
Mara nyingi si rahisi kutofautisha kati ya magaidi, wapinzani wa uhuru au watu wanaoendesha vita ya msituni. Hata jeshi rasmi za serikali zinaweza kutumia mbinu za kigaidi lakini kwa kawaida hawahesabiwi kati ya magaidi.

Mfano wa tendo la kigaidi


 

  • Tar. 9 Agosti 1998 kundi la Al-Qaida lililipuza mabomu kwenye balozi za Marekani mjini Nairobi na Dar es Salaam. Watu 223 walikufa na zaidi ya 4,100 walijeruhiwa. Kwa njia hii Al-Qaida ilitaka kupinga matendo ya Marekani katika Somalia. Kuna madokezo ya kwamba shabaha ya nyongeza ilikuwa kusababisha mashambulio ya Marekani dhidi ya Afghanistan ambako Al-Qaida ilikuwa na kimbilio. Lakini inasemekana ya kwamba viongozi waliogopa majadiliano kati ya makampuni ya Kimarekani na serikali ya Taliban nchini Afghanistan na mashambulio dhidi ya balozi zililenga kuvurugisha majadiliano yale hivyo kuimarisha kimbilio kwa Al-Qaida.
Kundi la Al-Qaida haikusikia uadui dhidi ya watu wa Tanzania au Kenya lakini haikusita kuwaua wengi kwa kutumiza shabaha yake ya kutisha serikali ya Marekani.

Post a Comment

 
Top