0



  Walimu wa shule za msingi manispaa ya Lindi wakiwa kwenye mafunzo ya STEP wanayoendeshwa na Taasisi ya elimu TEA
Elimu bure Halmashauri ya Kilwa,mkoani hapa Lindi inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo wazazi  na walezi kususia  kuchangia huduma za kielimu  na kusababisha shule nyingi kukosa  miundombinu mizuri,ikiwa ni pamoja na ukosefu wa vyoo ,madawati,vyumba vya madarasa na nyumba za kuishi watumishi wake.
 
Hayo yamebainishwa na wananchi wa kijiji cha Chumo wilayani Kilwa kwenye  kikao cha uhamasishaji elimu uliofanywa na wadau wa elimu kwenye Maazimisho ya juma la Elimu kitaifa lilofanyika wilayani humo kwa ufadhili (Tanzania Education Newtwork )Mtandao wa Elimu Tanzania TEN/MENT.
 
Akizungumza kwa niaba ya wananchi hao Jafari Lichingu  alisema hali ya elimu katika katika  kijiji na kata ya Chumo,siyo ya kuridhisha kutokana na changamoto zilizopo ambazo bado hazijaweza kupatiwa ufumbuzi wake ikiwemo elimu kwa wazazi  na walezi juu ya kauli ya elimu bure. 
 
Lichingu amezitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ukosefu wa vyoo,upungufu mkubwa wa madawati,vyumba vya madarasa na nyumba za kuishi walimu na vyooo kwa matumizi ya wanafunzi.
Alisema kutokana na mapungufu hayo, wanaiomba  serikali kuelimisha jamii  kuhusu maana ya elimu bure na kuwahamasisha wananchi kushiriki katika ujenzi wa madarasa,vyoo na nyumba za kuishi watumishi wa Idara hiyo.
Viongozi wakitoelimu  maana ya elimu bure  jamiii inaweza kubadilika  na kurudisha hali na  dhamira ya kujitolea  milango”Alisema Lichingu.
Kwa upande wake Kaimu Afisa Elimu wilaya Kilwa Salamu Nampoto alikiri kuwepo kwa  mkanganyiko wa kauli  ya elimu  bure   na elimu inahitaji kutolewa kwani  michango iliyoondolewa  ni ile inayo mgusa mtoto moja kwa moja kama vile ya uandikishaji.
Nampoto alisema michango inayogusa  jamii kuchangaia shule yao  haijafutwa  hivyo  ni wajibu wa wazazi na walezi  kuboresha shule zao kwa  kufanya  michingo  kwani shule  ni mali ya  jamii sio serikali.

Post a Comment

 
Top