Chama cha mpira wa miguu wilayani Liwale mkoani Lindi kupitia Kamati ya uchaguzi ya chama cha mpira wilayani Liwale (LIDIFA) imetangaza mchakato wa uchaguzi viongozi wa chama hicho.
Wadau wasoka wanaotaka kuwania uongozi katika chama hicho fomu zimeanza kutoka jana ijumaa tarehe 10.06.2016 na mwisho wa kurudisha fomu hizo ni tarehe 14.06.2016 fomu hizo zinapatikana kwa katibu wa kamati ya
uchaguzi ndugu Nardin kazumari.
Gharama ya fomu ni 100,000 na nyingine
50,000 kulingana na nafasi unayogombea huku kamati hiyo ikibainisha sifa ya kugombea ikiwa lazima uwe mtanzania mwenye
umri kuanzia miaka 18 mwenye akili timamu na uwe mjuzi katika mpira wa
miguu.
Fomu za shilingi 100000 zitakuwa katika nafasi 3 za Mwenyekiti,Makamo Mwenyekiti na Katibu Mkuu huku fomu za shilingi 50000 zitakuwa katika nafasi za wajumbe 3,mwakilishi wa vilabi,Katibu msaidizi na mweka hazina au Mwasibu.

Sifa nyingine ya kugombea uongozi huo ikiwa kuwa na elimu angalau ya kidato cha nne chenye
cheti cha ufahuru.
Uchaguzi wa kuwachagua viongozi unatarajiwa kufanyika namo siku ya jumamosi tarehe 16.07.2016
Post a Comment