Bahati Anthony akichezea kichapo.
Fundi nguo maarufu mjini hapa, Bahati Anthony aliyedai ni ‘wakala’ wa jamii ya siri inayohusishwa na utajiri wa ghafla na imani za kishetani ya Freemason, amenusa kifo baada ya kunaswa kwa utapeli kwa wakala wa mitandao yasimu inayotoa huduma ya kuweka na kutoa fedha.
Akiokolewa na polisi
Akisimulia tukio hilo, Assenga alikuwa na haya ya kusema: “Jana huyu jamaa alikuja hapa akatuma shilingi 15, leo amekuja ameniambia nitume laki tatu kwenye namba ileile aliyonipa jana.
“Baada ya kutuma, nimemwambia anipe hiyo laki tatu anadai yeye ni wakala wa Freemason hivyo baada ya dakika 10, begi alilobeba litajaa fedha na atanilipa. Nimesubiri dakika 10 zimepita.
“Nimemwambia anipe fedha zangu, anasema haijaingia, nikaamua kumpekua kwenye begi nikakuta mshumaa.”
“Wakati napekuwa ndipo akaanza kukimbia. Nilipoona nitapoteza fedha zangu, nikaona nimwitie mwizi ndipo watu wakamkamata na kumshushia kichapo.
“Nilipoona wanataka kumuua, nilikodi bodaboda na kumpeleka polisi ambako baada ya kuhojiwa alisema yeye siyo mwizi bali alielekezwa kufanya hivyo na kiongozi wa Freemason.
“Hata hivyo, polisi walimwamuru kurudisha fedha zangu ambapo aliwapigia simu ndugu zake kutoka Kigoma ambao walidai kuwa watanitumia fedha yangu ndipo aachiwe huru.”
Kwa upande wake, jamaa huyo aliyepokea kichapo alikuwa na haya ya kusema: “Nilisoma mabango ya Freemason yaliyozagaa mitaani yakihamasisha watu kujiunga, nilichukua namba za simu na kuwapigia ambapo waliniambia ili niwe tajiri natakiwa niwatumie shilingi elfu 15, nikatuma.
Kumekuwa na utapeli wa aina hiyo mkoani hapa hivyo Wikienda linawataka wasomaji wake kuwa macho ili wasilizwe.
Post a Comment