Zaidi
ya wafanyakazi arobaini na nne wanaofanya kazi katika kampuni ya
kichina ya Hainan Internation LTD inayojenga kituo cha kupokea na
kupooza umeme cha Singida hadi Shinyanga ,wamegoma kufanya kazi na
kuamua kuandamana hadi ofisi za idara ya kazi mkoani Singida, kwa
madai ya kutolipwa mapunjo ya mishahara zaidi ya shilingi milioni
themanini na laki saba.
Wafanyakazi hao wamesema wanadai haki zao zaidi ya mwaka moja na
wamesha peleka mashataka idara kazi mkoani Singida na hakuna hatua
zozote zinazo chukuliwa ,kwasababu wanapokwenda kupeleka malalamiko yao
baadaye naye meneja mradi huenda kwa Afisa idara ya kazi na hakuna
kinachoshugulikiwa.
ITV ilifika kumuona Meneja mradi wa kampuni ya Hainan Internation
LTD Bw. Ju Liang ambaye ni mchina hakuweza kupatikana mpaka tunaenda
mitamboni, lakini tulimkuta mmoja wa wafanyakazi wa kichina
aliyetambulika kwa jina moja la Bw. Yit naye alisema anadhani
wafanyakazi wamelipwa lakini tusubiri bosi ndiye atayejibu.
Kwa upande wake Afisa idara ya kazi mfawidhi mkoani Singida Bi.
Ruth Kalenga amekiri kuwa wafanyakazi wa kampuni ya Hainan Internation
LTD wanaidai kampuni hiyo na ametoa siku saba kuhakikisha madai yao ya
mapunjo ya mishahara inashugulikiwa.
Post a Comment