Wahanga
wa mafuriko wa mji wa Ifakara wilayani Kilombero wameiomba serikali
kuchukua hatua za makusudi kujenga tuta la mto Rumemo kufuatia mto huo
kuvunja kingo zake na kumwaga maji katika makazi ya wananchi na
kusababisha nyumba nyingi kuzingirwa na maji huku nyingine zikianguka
jambo linaloweza kusababisha mlipuko wa magonjwa mbalimbali ikiwemo
kipindupindu.
Baadhi ya waathirika wa mafuriko wilayani Kilombero wameendelea
kupata adha ya maji kufuatia nyumba zao bado kuzingirwa na maji jambo
linalosababisha kuendelea kuwafungia watoto ndani na wengine kuwapeleka
kwa ndugu zao ambapo wameomba serikali kuweka vifusi katika nyumba
zilizo zingirwa na maji pamoja na kujenga tuta la mto Rumemo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya yaKilombero Bw.Lephy Gembe amesema
serikali ipo katika mpango wa kuhakikisha wahanga wote wanapewa viwanja
pamoja na watu wanaoishi katika mazingira ya kujaa maji huku Mbunge wa
jimbo la Kilombero Peter Lijualikali akisema ipo haja ya kuhakikisha mto
Rumemo unajengewa tuta ili wananchi wa Ifakara waondokane na adha hiyo.
Post a Comment