0

Dodoma. Mkoa wa Iringa umetoa mkopo wa Sh437.4 milioni kwa ajili ya vikundi vya wanawake na vijana kwa kipindi cha 2015/16.

Hayo yameelezwa bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Seleman Jafo. amesema vikundi 430 vya wanawake vimefaidika na vya vijana ni 47.

Amesema Serikali inaendelea kuimarisha makusanyo ya mapato ya ndani kwa kutumia mfumo wa kielektroniki ili kuongeza mapato yatakayosaidia mifuko hiyo kutengewa fedha zaidi.

Jaffo alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Rose Tweve (CCM), ambaye alitaka kujua Serikali katika utaratibu wake wa kutenga asilimia 5 ya mapato yake kwa ajili ya wanawake na vijana, ilitoa kiasi gani kwa Mkoa wa Iringa na idadi ya vikundi vilivyonufaika.

Post a Comment

 
Top