Cape Verde wametua kileleni mwa orodha ya Fifa ya uchezaji kandanda barani Afrika ya mwezi Machi.
Huo ni ufanisi mkubwa kwa taifa hilo linalojumuisha visiwa kadha vidogo kaskazini magharibi mwa Afrika.Wamefanikiwa kuwapita mabingwa wa Afrika wa mwaka 2015 Ivory Coast ambao wameshuka hadi nambari mbili.
Cameroon pia wameimarika, na kuingia katika orodha ya 10 bora na kuwaondoa Guinea.
Licha ya kushinda Kombe la Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameshuka nafasi moja hadi nambari 58.
Miongoni mwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Uganda inaongoza ikiwa nambari 67, ikifuatiwa na Rwanda (85), Kenya (103), Tanzania (125), Burundi (129) na Sudan Kusini (140).
Mataifa yanayoshika mkia Afrika n Somalia, Eritrea na Djibouti, yote yakiwa nambari 204.
Duniani, Ubelgiji wanaongoza wakifuatwa na Argentina.
Hii hapa ndiyo orodha ya Fifa ya mataifa bora Afrika Machi:
- Visiwa vya Cape Verde
- Ivory Coast
- Algeria
- Ghana
- Tunisia
- Senegal
- Misri
- DR Congo
- Congo
- Cameroon
Orodha ya 10 bora duniani
- Ubelgiji
- Argentina
- Uhispania
- Ujerumani
- Chile
- Brazil
- Ureno
- Colombia
- England
- Austria
Post a Comment