0


Baadhi ya wananchi katika eneo la Tazara jijini Dar es salaam wamepongeza juhudi ambayo inaendelea kufanyika katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya juu yaani FLY OVER inayojengwa katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela j mradi ambao  utaghalimu kiasi cha shilingi bilioni 100 za Kitanzania.

Channel ten imetembelea katika eneo la Tazara na kushuhudia Kampuni iliyopewa  tenda ya kujenga barabara hiyo ikiendelea na zoezi la Uchimbaji wa barabara ikiwa ni hatua ya pili ya ujenzi katika ukamilishaji wa Mradi huo Tangu ilipozinduliwa na Rais  wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli.

Wakitoa maoni yao baadhi ya wananchi hao wameeleza kuridhishwa na mwenendo mzima wa hatua ya ujenzi wa barabara hiyo ambapo wamesema umezingatia mambo mbalimbali ikiwemo Suala la Usalama barabarani kwa kuweka alama maalum kwa watumiaji wa barabara ya Nyerere na Mandela.

Kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la msongamano wa magari katika jiji la Dar es salaam na kuwarahisishia wananchi kufanya shughuli zao kwa haraka.

Mradi huo unatekelezwa na serikali ya Japan kupitia shirika la msaada la Japan – JICA,  kwa kupitia kampuni ya kimataifa ya ukandarasi ya Sum Tomo na unatarajiwa kukamilika mwezi oktoba mwaka 2018.

Post a Comment

 
Top