Afisi za shirikisho
la soka barani Ulaya Uefa zimevamiwa na maafisa wa polisi wa Uswizi
baada ya aliyekuwa katibu mkuu Gianni Infantino ambaye sasa ni rais wa
Fifa kutajwa katika stakhabadhi zilizofichuliwa na kampuni moja ya
mawakili wa Panama Mossack Fonseca.
Imebainika kwamba Infantino
alikuwa mmoja ya watu watatu waliotia saini kandarasi za haki za
kupeperusha moja kwa moja matangazo ya mechi za vilabu bingwa Ulaya
runingani mwaka 2006.Watu hao wawili ambao ni wafanyibiashara wametuhumiwa na madai ya kutoa hongo
Infantino hatahivyo amekana kufanya makosa yoyote.
Post a Comment