0
 
Trump na Senecal
Huduma ya ujasusi ya Marekani imeanzisha uchunguzi baada ya aliyekuwa muhudumu mkuu wa nyumbani kwa Donald Trump kutaka rais Barrack Obama auawe.
Anthony Senecal aliandika katika mtandao wake wa Facebook kwamba Obama angechkuliwa na jeshi na kupigwa risasi kwa kuwa adui katika muhula wake wa kwanza.
Bwana Senecal alimfanyia kazi bwana Trump,mgombea wa urais kupitia chama cha Republican kwa takriban miaka 30.
Kampeni ya Trump hatahivyo ilijiepusha na matamshi ya Senecal.
''Hakuajiriwa na Trump na hajaajiriwa tangu mwezi Juni 2009'', alisema msemaji wa kampeni ya Trump Hope Hicks katika taarifa.
 
Obama
''Tunashtumu matamshi haya machafu kutoka kwa Senecal.Chapisho hilo la Bwana Senecal halikuwa hadharani.
Na baadaye siku ya Alhamisi, bwana Senecal mwenye umri wa miaka 84 alikiambia chombo cha habari cha CNN kwamba Obama anafaa kunyongwa nje ya Ikulu ya White House.
Pia aliitaja Ikulu ya White House kuwa ''msikiti mweupe''.BBC

Post a Comment

 
Top