Serikali ya
Tanzania imewahakikishia wakaazi wa jiji la Dar es Salaam kwamba
inatatua tatizo la uhaba wa maji mjini humo na hivi karibuni tatizo hilo
litakuwa historia.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini
Tanzania,naibu waziri wa maji na unyunyizaji Bw Issack Kamwelwe amesema
kuwa serikali kwa sasa imeanzisha mradi wa kuimarisha usambazaji wa maji
katika maeneo ya mji yanayokumbwa na uhaba mkubwa wa maji.
Kulingana
na Bw Kamwele,mradi huo ambao una thamani ya dola milioni 32.9 na na
unaotarajiwa kukamilika mwezi Aprili mwaka 2017 unashirikisha
kubadilisha mabomba ya zamani,na kuweka mapya na kuweka mabomba mapya
maeneo ambayo hayajaangaziwa.
Baadhi ya maeneo ambayo yatafaidika
na mradi huo ni mji wa
bagamoyo,Mpiji,Bunju,Mabwepande,Boko,Bweni,Tegeta,Ununio,Wazo,Salasala,Kizundi,matosa,Mbezijuu,Goba,Changabyikeni,makongo,Kiluvya,Kibamba,Mbezi,Msakuzi,Mkabe,Maramba
Mawili na Msigali.
Post a Comment