0

Mbunge wa Tabora Mjini Emmanuel Mwakasaka amehoji bungeni juu ya kutokuwepo kwa kiwanda cha sigara katika Mkoa wa Tabora pamoja na jitihada za wananchi kulima sana zao la tumbaku na kuliingizia taifa mapato.

Akijibu swali hilo Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe Charles Mwijage amesema kamba tayari serikali imepata mwekezaji raia wa China ambaye atakwenda kukagua eneo hilo na mambo yakienda sawa kiwanda hicho kitajengwa.

''Wabunge wa Mkoa wa Tabora Jumamosi twendeni Tabora ili Jumapili tuonane na mwekezaji na kama hakutakuwa na mambo ya ajabu kuhusu kupatiwa eneo la ardhi kiwanda hicho kitajengwa''- Amesema Waziri Mwijage.

Aidha Waziri huyo amewaambia wabunge kuwa Mbunge ambaye atamchangamkia katika kushughulikia eneo lake basi na yeye atamchangamkia katika kutatua kero zao.

Post a Comment

 
Top