Mwanamke aliyetambuliwa kuwa mkongwe zaidi duniani ameaga dunia akitibiwa jijini New York, Marekani, madaktari wamesema.
Susannah Mushatt Jones, amefariki akiwa na umri wa miaka 116.Alizaliwa eneo la mashambani jimbo la Alabama mwaka 1899, na amekuwa akiugua kwa siku kadha.
Mwanamke Mwitaliano, Emma Morano, ambaye ni mdogo wa umri wa Bi Jones kwa miezi kadha, sasa ndiye anayetambuliwa kuwa mwanamke mkongwe zaidi duniani.
Anaaminika kuwa mtu pekee duniani aliyezaliwa karne ya 19 ambaye bado yuko hai.
Post a Comment