Timu ya Taifa ya
vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya Tanzania maarufu kama Serengeti
Boys imetua jijini Goa, India kwa ajili michuano maalumu ya soka ya
kimataifa kwa vijana (AIFF Youth Cup 2016 U-16) yaliyoandaliwa na
Shirikisho la Soka nchini humo (AIFF).
Michuano hiyo inatarajiwa
kuanza leo Mei 12, 2016 kwa mfumo wa ligi kwa timu tano kucheza mechi
nne, Tanzania itafungua dimba dhidi ya Marekani kwenye Uwanja wa Tilak
Maidan, Vasco, Goa huku mchezo wa pili ukiwa kati ya wenyeji India dhidi
ya Malysia Mei 15, mwaka huu.
Serengeti Boys watashuka dimbani
tena Mei 17, kucheza na wenyeji India mchezo wa kwanza, Mei 19 Serengeti
Boys watacheza dhidi ya Korea Kusini na mchezo wa mwisho watamaliza
dhidi ya Malaysia Mei 21.
Fainali ya michuano hiyo itachezwa Mei
25 ambapo kabla ya mchezo wa fainali, utachezwa mchezo wa mshindi wa
tatu katika uwanja huo huo Tilak Maidan, Vasco, Goa nchini India.
AIFF
kimeandaa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ikiwa ni
sehemu ya maandalizi ya kikosi chao kwa ajili ya Fainali za Kombe la
Dunia kwa Vijana zitakazofanyika nchini humo mwaka 2017.
Post a Comment