Ripoti ya siri
iliyowasilishwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa inaituhumu
Rwanda kwa kuendelea kuwasaidia waasi wanaotaka kumtoa madarakani Rais
wa Burundi Pierre Nkurunziza.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Rwanda imekuwa ikitoa mafunzo, ufadhili na usaidizi wa kimipango kwa waasi hao.Baadhi ya maafisa wan chi za Magharibi wamekuwa wakidhani hilo lilikoma baada ya kutolewa kwa ripoti nyingine mwaka jana, lakini ripoti hiyo inasema hali ni kinyume.
Kamati ya Baraza la Usalama la UN inayoshughulika na vikwazo itajadili ripoti hiyo baadaye leo Ijumaa.
- Rwanda kuwahamisha wakimbizi kutoka Burundi
- Rwanda lawamani juu ya Burundi
- Rwanda yapuuza madai ya ujasusi ya Burundi
Rais Nkurunziza alichaguliwa kwa muhula wa tatu mwezi Julai mwaka jana.
Jaribio la mapinduzi lilitekelezwa mwezi Mei lakini halikufanikiwa.
Post a Comment