MKUU wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekipongeza kituo cha redio cha EFM
kwa kuanzisha shindano lijulikanalo kama ‘Shika ndinga na EFM’, lenye
lengo la kuwasaidia wananchi wa hali ya chini na kati katika kujikwamua
na umaskini.
Akizungumza
hivi karibuni wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano hilo,
Makonda alisema shindano hilo ni zuri na linamanufaa kwa wananchi kwani
halina chembe ya wizi bali ni nguvu na akili ya mtu ndo uhitajika ili
kuweza kushinda.
“Naishukuru
sana EFM kwa kuanzisha shindano hili kwani nilivyoliona si la wizi ni
shindano ambalo linamtaka mshiriki kutumia akili yake na nguvu zake ili
kuweza kushinda, hivyo basi nawaomba wananchi washiriki katika mambo
ambayo yanamanufaa kwao na si yale yanayowapotezea muda,” alisema
Makonda.
Hata hivyo
Makonda amewataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuendelea kuzingatia
suala la usafi na kutambua kuwa usafi ni jambo la muhimu katika maisha
ya kila siku.
Fainali ya
shinda ndinga na EFM wamefikia tamati na kupatikana kwa washindi wawili
waliojishindia gari aina ya Keri mahususi kwa kubebea mizigo.
Post a Comment