Aliyekuwa waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza , David Miliband, ametoa wito wa kufungwa kwa kambi zote za wakimbizi duniani.
Bwana
Miliband, ambaye ni rais wa kamati ya kimataifa ya uokozi,anasema kuwa
wakimbizi wanafaa kufanywa raia wa mataifa wanamoishi na kupewa haki ya
kufanya kazi.Akiongea kabla ya kongamano la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadam, Miliband amependekeza asilimia kumi ya wakimbizi milioni 60 duniani, walio katika mazingira magumu, wapewe hifadhi na mataifa tajiri duniani.
Post a Comment