Mstahiki
Meya wa Ilala Mh.Charles Kuyeko amemwagiza Mganga Mkuu wa halamashauri
ya Ilala Bi.Victorina Ludovick kuwachukulia hatua kali wauguzi watatu
waliofanya uzembe na kusababasha kifo cha mwendesha bodabada Nasoro
Hamisi aliyepigwa risasi na majambazi.
Akizungumza na vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam leo amesema
haiwezekani kuwavumilia watumishi wa serikali wazembe na wanaokiuka
maadili ya kazi.
Naye Filbert Gikanka ambaye alimkimbiza hospitalini marehemu Nasoro
Hamisi katika hospitali ya Amana amesema mhudumu wa zamu alikataa
kumpokea mgonjwa aliyekuwa anavuja damu nyingi na kutaka alipwe fedha
shilingi elfu ishirini ili damu ipatikane na mgonjwa aliendelea kuvuja
damu nyingi na hatimaye kufariki baada ya muda mchache.
Post a Comment