0
               
   
 Timu ya Kigamboni fc yaendelea kung'aa baada ya kuibuka ushindi wa goli 1 bila dhidi ya Kombaini fc katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa shule ya Msingi muungano.

Goli pekee la kigamboni fc lililoipa ushindi lilifungwa na Ramadhani mtunage goli liliofungwa  katika dakika ya 25 kipindi cha kwanza na kupelekea mpaka mchezo unamalizika dakika 90 matokeo yalikuwa Kigamboni 1 na Kombaini hawajapata kitu.

Kigamboni moja ya timu ambayo haijawahi kupoteza mechi hata moja toka waanze mashindano haya april 27 matokeo Likongowele 1-3 Kigamboni,may 5 Kigamboni 5-1 Nangando,may 11 Kombaini 0-1 Kigamboni  huku ikisubiria mchezo mmoja kukamilisha mzunguko may 17 kutakuwa na mechi yao ya nne kati ya Z fc Vs Kigamboni.

Ligi hiyo ya Mbuzi vijana cup inayoendelea wilayani Liwale itaendelea tena hapo kesho katika mchezo utakaokutanisha  timu ya Kubota fc Vs Wakaanga sumu fc.

Post a Comment

 
Top